Ezekiel 11:3-6

3 aWao husema, ‘Je, hivi karibuni hautakuwa wakati wa kujenga nyumba? Mji huu ni chungu cha kupikia, nasi ndio nyama.’ 4 bKwa hiyo toa unabii dhidi yao, tabiri, Ewe mwanadamu.”

5 cKisha Roho wa Bwana akaja juu yangu, naye akaniambia niseme: “Hili ndilo Bwana asemalo: Hili ndilo ninyi mnalosema, ee nyumba ya Israeli, lakini ninajua mnalowaza mioyoni mwenu. 6 dMmewaua watu wengi katika mji huu na kujaza barabara zake maiti.

Copyright information for SwhKC